Mashirika Pwani Yazindua Kampeni Kuzima Moto Korona Shuleni

Mashirika ya kijamii katika kaunti ya Mombasa yamezindua rasmi kampeni ya kudhibiti msambao wa virusi vya korona  katika taasisi mbalimbali ukanda wa pwani

Kaunti ya Mombasa Ikiwa katika harakati ya kudhibiti maambukizi zaidi yanayokithiri baada ya shule ya upili ya Star Of the Sea pamoja na ile ya Tononoka kuripoti visa vya korona wiki chache zilizopita

Kulingana na mwalimu mkuu katika shule ya frère town eneo bunge la Nyali katika kaunti hiyo suala la  uvaaji maski bado linasalia kuwa changamoto miongoni mwa wanafunzi jambo ambalo linachangia maambukizi zaidi shuleni.

Haya yanajiri takriban wiki tatu baada ya shule ya Tononoka kumpoteza mwalimu mkuu kutokana na virusi hivyo

Gavana wa Kaunti ya Kilifi Amason Kingi ametishia kufunga mipaka yake baada ya wanafunzi 38 wa shule ya upili Marafa kuambukizwa virusi hivyo mapema leo huku wanafunzi hao wakitengwa katika chumba tofauti na wenzao.

Hata hivyo wito umetolewa kwa wazazi na wanafunzi kutilia maanani kanuni zilizowekwa na wizara ya afya kudhibiti msambao zaidi wa korona huku kampeni hiyo ikilenga kufikia shule zote kanda ya pwani.

https://choupsee.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287