Madaktari Chini ya KMPDU watishia kugoma,

Madaktari wametishia kushiriki mgomo baada ya ongezeko la idadi ya madaktari na wahudumu wa afya kuambukizwa virusi vya korona.

KMPDU imetoa ilani ya siku 21 kwa serikali kushughulikia matakwa yao la sivyo hakuna daktari   atakaye hudumia wagonjwa .

Kulingana na Katibu mkuu Chibanzi Mwachoda , madaktari hawajapokea marupurupu kwa miezi 8 ,magwanda ya kazi( PPEs) hazitoshi hivyo basi hakuna daktari atakaye hatarisha maisha yake kwa sababu ya uzalendo.

Mwakilishi wa madaktari kusini mwa bonde la ufa Daphry Achela amesema kuwa madaktari wanaumia na wanateseka kwani wanahisi kuwa wamekataliwa na serikali kuu na ile ya  kaunti huku hofu ya kuambukizwa covid-19 ikiwazonga baada ya bima ya afya NHIF na bima nyingine kukataa kugharamia  wagonjwa wa virusi hivyo nchini.

Bwana Achela amesema pia kaunti kama ya narok, kajiado na laikipia zina upungufu wa madaktari na wahudumu wa afya aidha Chibanzi anadai kutengwa na serikali

 

https://ptirtika.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287