Amnesty International yaitaka Kenya kutomfukuza mwanasiasa mpinzani wa Tanzania

Mtanzania Godbless Lema Picha kwa hisani

Shirika la Amnesty International limekashifu hatua ambayo serikali ya Kenya inataka kuchukua ya kumfukuza nchini humo mwanasiasa wa upinzani wa Tanzania GodBless Lema na familia yake ili kufunguliwa mashtaka nchini Tanzania.

GodBless Lema alikamatwa Jumapili ya Novemba 8, 2020 baada ya kuvuka mpaka wa Kenya na Tanzania huko Namanga kwenye kaunti ya Kajiado nchini Kenya akiwa na nia ya kupata hifadhi kutoka serikali ya Kenya.

Mkurugenzi mtendaji wa shiriko hilo Irungu Houghton amesema kuwa Kenya sharti isikiuke sheria za kimataifa zinazolinda watu wanaotafuta hifadhi nchini na kuwarudisha nchini mwao ambapo kuna kila sababu ya wao kufunguliwa mashtaka na maisha yao kuwa hatarini.

Ameongezea kuwa kuhamishwa kwa Lema kutasababisha kukiukwa kwa haki zake. Wakili wa Godbless Lema Profesa George Wajackoyah amedhibitisha uwezekano wa Lema kurudishwa Tanzania.

Shirika hilo limesema kuwa Lema yuko na haki ya kusikizwa na uamuzi kutolewa kuhusu ombi lake.

 

 

 

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287