Wana Afya Watishia kugoma Iwapo Serikali Haitotekeleza Matakwa yao

Health care workers stage a protest during the ongoing doctors' strike in Kenya.
wahudumu wa afya tawi la Mombasa wameitaka Serekali kutilia mkazo mishahara ya wauguzi ya tangu mwezi wa pili mwaka huu
Kulingana na kauli ya Kiongozi wa chama hicho Franclin makanga, hadi kufikia sasa wauguzi hao hawajapata mishahara yao kwa wakati upasao.
Aidha Franclin amesema kuwa wataendelea na mgomo iwapo hawatapokea mishahara yao ipasavyo hadi pale serekali itakapo timiza matakwa yao .
Vile vile wahudumu hao wamebainisha kuwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya korona miongoni mwao na raia nikutokana na upungufu wa vifaa hitajika kujikinga dhidi ya COVID-19 katika hospitali za kaunti ya Mombasa.
Hata hivyo Wito umetolewa kwa wizara ya leba pamoja na tume ya kuratibu mishahara kuweka katika gazeti la serikali COVID-19 kama gonjwa linaloathiri ajira zote