Pigo! Mwalimu Mkuu wa Shule ya Tononoka Afariki kutokana na COVID-19,Mombasa.

Biwi la simanzi limegubika shule ya upili ya tononoka mjini Mombasa baada ya kumpoteza mwalimu mkuu wa shule hiyo Mohamed Khamis mapema hii leo.

Akithibitisha taarifa hiyo naibu mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema kuwa kifo chake kinajiri siku chache baada ya kuthibitishwa kuugua virusi vya korona na kupelekea kufungwa kwa shule ya Tononoka kwa muda wa wiki mbili.

Shule hio ya tononoka Pamoja na star of the sea zilifungwa Juma tano wiki iliyopita baada ya kuripoti visa 15 vya maambukizi ya virusi vya Korona huku marehemu Mohammad Khamis akiwa miongoni mwa walioambukizwa.

Tukio hili linajiri wiki chache baada ya agizo la waziri wa elimu Pro. George Magoha kufungua tena shule tarehe 12 mwezi Oktoba zilizokuwa zimefungwa ili kudhibiti msambao wa virusi vya korona.

Hata hivyo wizara ya afya imeshuhudiwa ogezeko la maambuki hayo muda mchache tu baada ya ufunguzi huo nchini.