KMYA Yaadhimishwa kwa Njia ya Kipekee Siku Ya Mwanamke Kijijini.

Wanawake  kijijini wameweza kuungana na kubuni chama cha akiba na kupeana  mikopo katika viviji vyao ili kuimarisha uchumi wao na kuweza kulea watoto wao.

Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya mwanamke wa kijijini ulimwenguni, Shirika la kenya muslim youth alliance (KMYA) imepata fursa ya kuungana na mama Rukia Juma kutoka Kijiji cha Mwandimu kaunti ya Kwale ili kuadhimisha siku hii ikiwa kauli mbiu ni kujenga udhibiti wa mwanamke kijijini katika kukabiliana na janga la korona.

Mama Rukia ameweza kueleza changamoto zinazowakabili wanawake wa kijijini zikiwemo kuzorota kwa uchumi na biashara, majukumu ya malezi, afya hafifu ya uzazi, ukosefu wa usalama, uongozi uso bora nakadhilika.

Hata hivyo Mama Rukia amependekeza viongozi wa kitaifa, kaunti na washika dau wengine kuleta huduma na mikopo ya kinama ikiwemo Uwezo funds, women enterprise fund na zenginezo vijijini ili waweze kuboresha maisha yao.