Kijana Ashtakiwa Mahakamani kwa Kumtusi Babaye Mtandani
Kijana mmoja ameshtakiwa Katika mahakama ya Mombasa Hii leo kwa madai ya kutumia mtandao wake wa simu kusambaza ujumbe wa matusi kwa babake mzazi.
Rajab Hamisi anadaiwa kutuma ujumbe wa matusi na chuki baada ya kukosana na mzazi wake mwezi Juni mwaka huu jambo ambalo lilimkera babake kiasi cha kumshtaki ,aidha babake mshukiwa ambaye amekuwa mahakamani ameelezea mahakama kuwa yuko radhi kumsamehe mtoto wake iwapo atamwomba msamaha.
Hakimu Ritah Amwayi amewapa baba na mwanawe wiki mbili kurudisha uhusiano huku mshukiwa akiachiliwa kwa dhamana ya pesa taslim elfu 50.
Kesi hiyo itatajwa 26 mwezi huu