Sumu ndani ya Vitabu!

By: Ahlam Majid

 

Kulingana na utafiti, takriban asilimia 70 ya wanafunzi wa vyuo vikuu na vile vya anuwai hupoteza nyakati zao  mwingi kushiriki starehe na anasa bila kuzingatia muda wao wa kusoma wengiwakipuzilia mbali mazoezi ya darasani na mitihani ya kozi zao.

Utafiti huo uliofanywa na shirika moja lisilo la kiserikali kati ya Januari na Machi 2020, katika vyuo mbali mbali Kaunti ya Mombasa, wanafunzi wenye umri wa miaka kati ya  20-30 huzuru vyumba vya burudani na vilabu maarufu mjini kujivinjari kwa kubugia vileo na kusakata densi hasa bila kuwajibikia masomo yao.

Kulingana na vyombo vya usalama, sherehe kama hizi huchangia sana ukosefu wa usalama kwani wengi wao huvamiwa na kuporwa wanapokuwa humo vilabuni ama njiani kurejea vyuoni, wengine hata kuripotiwa kutoweka, maiti zao zikipatikana baadaye.

Aidha wanafunzi waliohojiwa wanahisi kuwa wanapokuwa vyuo vikuu, wanahitaji uhuru wao wa kutenda wapendavyo bila kuwekewa usimamizi wa aina yoyote.

Tumelindwa na wazazi tukiwa shule za msingi hadi shule za upili, sasa tuko chuo kikuu, tuachwe tujilinde aise, ujana ni moshi jamani” Alikiri mwanafunzi mmoja.

Sisi tumekomaa, tunajua tunachofanya, hapa  tumekuja kusoma, kando na hayo maisha ni yetu binafsi” Akaongezea mwenzake wa kike

Aidha wazazi na walimu waliohojiwa walikuwa na maoni tofauti .

“Kukorofika kwa mtoto lazima mzazi ajukumike kumkosoa , kwani mtoto kwa mzazi hakui” Alisema  Ali Mahadhi, mzazi wa mwanafunzi wa chuo cha  Pwani.

“Mwanangu tangu ajiunge na chuo kikuu simtambui mimi, amekuwa tofauti saana, si wa kutumwa wala wa kukanywa kama awali” Alisema Mwana Mausa kwa machungu.

Kulingana na matokeo ya ripoti hiyo, mapuuza  kwa masomo miongoni mwa wanafunzi vyuoni husababisha wengine kufeli kuhitimu kozi zao, wengine wanahitimu na  matokeo yenye viwango vya chini sana inayowapa chanagamoto kujipatia kazi, huku nao waajiri wakilalamikia  ukosefu wa ueledi hitajika kwa baadhi ya waajiriwa wapya kutoka vyuoni.

https://vaugroar.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287