Ajuta kutaka kujitoa Uhai baada kuavya mimba Likoni , Mombasa
Mahakama ya Mombasa imemuhukumu msichana mmoja baada ya kukiri kosa la kutaka kujiuwa katika kituo cha polisi cha Likoni.
Mahakama imeelezwa kuwa Zainabu Mwachirumbi awali alizuiliwa katika kituo cha Likoni kwa madai ya kuavya mimba kisha akatoweka kuelekea msalani na kujaribu kujinyonga kabla ya kuzuiliwa na polisi waliokuwa wakishika doria.
Aidha ripoti ya kurekebisha tabia imebaini mshtakiwa alitenda kitendo hicho akiwa katika akili zake timamu huku mshukiwa akiomba msamaha kwa kitendo hicho