Shujaa Anayetumia Silaha Ya Rangi Kuangaza Jamii

Ulingo wa sanaa unakuwa huku nafasi zikitokeza kila uchao wengi wakitumia fursa hii kukabili janga la virusi vya korona nchini.

Firdaus Ahmed msichana mwenye umri wa mika 19 amejitwika katika ulingo wa sanaa ya uchoraji baada ya kuijaribu na kupenda kuanzia shule ya upili kabla ya kujiunga na kampuni urembo na muonekano wa ndani Dubai

Kulingana na firdaus tasnia hii ya uchora alojitolea kuifanya  inatawaliwa na wanaume akiwa katika mstari wa mbele kukuza jinsia ya kike na kauli mbiu ‘what a man can do a woman can do better’, ila bado wengi katika wanawake hawajaikubali wala kuijaribu.

Hata hivyo kama tasnia nyingine nchini firdaus amekumbwa na changamoto kadha wa kadha kujiendeleza na kukuza kupaji chake cha uchoraji. Ukosefu wa vyuo vya ukufunzi wa sanaa ya uchoraji ikimpelekea kusaka mwangaza katika mataifa ya nje pasi na kukata tamaa hivyo kujipatia elimu zaidi ya sanaa hii adimu barani Afrika.

Kwa upande mwingine ukosefu wa soko kwa kazii hii inavunja moyo kwani inamlazimu mwanadada huyu kununua baadhi ya vifaa kutoka mataifa ya nje ili kuhakikisha kazi yake ni bora na kufano wa kuigwa katika jamii. Vifaa vingi katika kaunti ya Mombasa anamoishi ni duni na baadhi kukosekana kabisaa.

Kama shilingi kuwa na pande mbili sanaa hii imemletea manufaa Firdaus ikiwemo kutangamana watu kutoka tabaka mbali, kuzuru mataifa kadhaa kando na kujipatia kipato kiasi kutokana na talanta hii yake iliyo adimu kwa jamii ya kike.

Kwa sasa Firdaus anahamasisha vijana hasa kina dada kujikuza kisanaa na kupenda kazi zitokanazo na talanta zao huku akijihusisha kufundisha baadhi kupitia mitandao mbali mbali ikiwemo Instagram.