Shunguli za Ukombozi Kuendelea , Hofu Ya vifo zaidi

Wafanyakazi wa uokozi wanaendelea kuwatafuta watu waliofukiwa kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka, siku moja baada ya mlipuko mkubwa kutokea katika bandari ya Beirut na kuwauwa Takriban watu 100.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Lebanon limesema kuwa karibu watu 4,000 wamejeruhiwa na huenda idadi ya vifo ikaongezeka. Afisa mmoja wa ulinzi wa kiraia akisema bado wanawatafuta karibu watu 100 waliofukiwa kwenye vifusi, hasa karibu na bandari ya Beirut.

Walebanon wameamka leo na kushuhudia uharibifu mkubwa uliotokea katika bandari hiyo pamoja na maeneo ya karibu katikati mwa mji huo mkuu.

Wafanyakazi wanaendelea kuondoa vifusi ili kufungua barabara na kukarabati maeneo yaliyoharibiwa. Baraza la Mawaziri la Lebanon linatarajiwa kufanya kikao cha dharura leo baada ya Baraza Kuu la Ulinzi la Lebanon kuitangaza Beirut kuwa eneo la janga na kupendekeza hali ya hatari kwa wiki mbili.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287