Arsenal na Chelsea kukabana koo Fainali ya FA, Wembley

LEO HAPATUMWI MTU DUKANI!

Nani atabeba ubingwa wa FA? Picha kwa Hisani ya Skysports

Nyasi zitaumia mwendo wa Saa Moja Unusu jioni (7.30PM) majira ya Afrika Mashariki pale Wababe na wapinzani wa jadi wa mjini London Arsenal watakapokabana koo na Chelsea uwanjani Wembley.

 

Ni katika mchuano wa Fainali ya Kombe la FA nchini Uingereza ambapo Washika Bunduki maarufu (The Gunners) Arsenal chini ya ukufunzi wake Mikel Arteta watamenyana na vijana wa Samawati (The Blues) Chelsea wanaonolewa na mkufunzi Frank Lampard.

 

 

Patashika nguo kuchanika inatarajiwa kujiri leo jioni ambapo wakufunzi wote wawili watapigania taji hilo kwa mara ya kwanza chibi ya uongozi wao ambapo mameneja wote hao wakiwa katika mwaka wao wa kwanza wa ukufunzi.

 

 

Klabu ya Arsenal ambayo ndyo klabu iliyoshinda mataji mengi zaidi ya FA katika historia wanajibwaga uwanjani leo kusaka taji la 14 huku Chelsea nao wakisaka taji la 8.

kwa pamoja Arsenal na Chelsea wametawala dimba hilo la FA katika kipindi cha miaka 20 sasa huku timu zote zikishinda taji hilo mara 6 katika kipindi hicho.

 

Kikosi cha mashambulizi cha Arsenal kinatarajiwa kuongozwa na nahodha wao Pierre Emerick Aubameyang akishirkiana na Alexandre Lacazatte huku Chelsea nao wakitarajiwa kuongozwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal mfaransa Olivier Giroud na Mmarekani Christian Pulisic.

 

Nani atabeba ubingwa huo? Muda ndio utakaosema.

 

 

https://upskittyan.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287