Unyanyasaji wa Kijinsia Kukithiri Pwani

Kaunti za Kwale na Kilifi zimekuwa kwenye ramani kwa muda mrefu Sasa na kuoteshwa vidole kama kitovu cha uchafu wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto.

Kesi hizi mara nyingi  humjumuisha asiye na sauti na jamaa wa karibu wa familia ambaye kwa njia moja au nyingine hutishia mtoto huyu asiye na usemi asitoe ripoti kama hizo hadharani.

Hata kama serikali na mashirika mengine yasiyokuwa ya kiserikali yanajizatiti na kuongoza kushughulikia kesi hizi  kuhakikisha kuwa wahalifu wanachukuliwa hatua, wanashauriwa na kuwa katika uangalizi mzuri, bado kumekuwa na pengo katika kushughulikia suala hilo kwa misingi ya kiafya.

Kwa miaka mingi, vijana ambao hupata shida za kutisha mikononi mwa waliowanyanyasa, wameachwa na makovu michubuko mioyoni mwao na akilini, maumivu ambayo hayatoweza kutoweka.

Makala haya yanapiga darubini changamoto zinazowakumba, hali ya kutengwa na jamii bila kusahau Unyanyapaa .

Usikose kutembelea tovuti hii kwa makala haya kwa kina

mwandishi; Munna