Makali ya Wembe yahatarisha Maisha, Wasichana wachanga Nchini.

Ukeketaji unazidi kuzua changamoto za kiafya kwa jamii yakike na kupelekea utumizi wa raslimali nyingi za nchi na katika vita ndidhi ya madhila hayo katika jamii.

Katibu mwandamizi katika wizara ya vijana na Jinsia Rachael Shebesh amesema kuwa  wasichana wadogo wanazidi kukeketwa licha ya kampeni hizo kali kufanywa katika kaunti mbali mbali nchini.

Akizungumza katika kaunti ya Taita Taveta,Shebesh amesema kuwa baadhi ya wazazi wanashirikiana na kina nyanya na wazee ili kutekeleza ukeketaji huo hususan kwa watoto wadogo.

kulingana na shirika la afya duniani WHO, wanawake na wasichana waoathirika na ukeketaji wanakabiliwa na hatari kubwa katika afya yao na saikolojia kwa jumla, hii ikiwa ni pamoja na athari zinazochipuka  pindi tu baada ya kukeketwa ikiwemo maambukizi ya virusi vya HIV, kuvuja damu kupita kiasi au shida ya wasiwasi pamoja na magonjwa ya kudumu ambayo huenda yakamtokea aliyekeketwa maishani.

Baadhi ya wasichana wanaokeketwa wana uwezekano mkubwa wa kupata tishio la kupoteza maisha yao wakati wa kujifungua vile vile kukumbwa na magonjwa ya kuambukizwa. Wakati mwingi waathiriwa wa madila haya huhisi uchungu wakati wa hedhi, wakienda haja ndogo au wakati wa kitendo cha kujamiana, changamoto zinazowakosesha raha na uhuru maishani.

Hata hivyo Shebesh ameahidi kushirikiana na polisi, machifu pamoja na mabalozi wa nyumba kumi huku akiongeza kuwa kila mtoto wa kike atakayepelekwa kliniki atakuwa akiangaliwa na madaktari ikiwa amekekeketwa au la akionya kuwa mzazi yoyote atakayepatikana mtoto wake amekeketwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287