Suluhu kwa utata wa ugavi wa fedha za kaunti

Utata miongoni mwa maseneta bungeni kuhusu mfumo bora na isiyo na mapendeleo katika ugavi wa fedha kwa kaunti zetu unaendelea kuzua taharuki miongoni mwa wananchi, Magavana nao wakitangaza kufilisika kwa akiba ya kuendesha shughuli za kaunti.

Tuanze hivi;

Itakuchukua siku kadhaa kuzuru kaunti ya Mandera, vilevile itakuchukua wiki nzima kuzuru kaunti ya Marsabit, lakini kumbuka itakuchukua kama siku moja tu, ikienda sana siku mbili kuzuru kaunti nzima ya kiambu, kile ambacho maseneta hawa wanavutania, ni idadi ya wanaotaka huduma kwa kaunti hizi, bila kujali ukubwa wala udogo wao, wengine wanamtazamo wa ukubwa wa eneo, wengine wanataka kuzingatiwa kinachopatikana katika kaunti zetu, aina gani ya kilimo, viwanda n.k.

Mjadala huu unatukumbusha mvutano uliokuwepo awali ya one man, one shilling, one vote, dhidi ya mjadala wa one man, one kilometer one shillings.

Kwa kuwa wale ambao wanatoka maeneo pana wanahoji kuwa inatuchukua muda kupeleka huduma, wakati wanaotoka maeneo ndogo na watu wengi, wakihoji kuwa , wanajilazimisha kuwahudumia watu wengi kila siku bila kupumzika.

Nahisi kuwa, ili kuleta umoja, tungeanza kuwa na mtazamo tofauti kando na jinsi ya  kugawanya keki na badala yake kuanza kuoka keki kubwa ili pesa ziwe zinapatikana kwa kila kaunti kwa urahisi.

Iwapo mfumo huu utapitishwa, kaunti ya Mandera itapoteza shilingi bilioni 2, Wajir itapoteza bilioni 1.4, Kwale bilioni 1.2, Kilifi bilioni 1.1, Marsabit milioni 984, Narok milioni 853, Mombasa milioni 682, Makueni milioni 574 , Nyamira milioni 560 Tana River milioni 499, Tharaka Nithi milioni 499, Garissa milioni 484 Kuna kaunti 19 ambazo zitapoteza pesa na kaunti 28 zitaongezewa pesa.

Hapa pia kuna swala la kisiasa, na vilevile swala la Handshake, kisha kuna swala la uchaguzi wa 2022, Kwa sababu, sheria inasema, ili utangazwe mshindi wa kiti cha urais, lazima upate angalau asilimia 25 za kura zilizopigwa kwa angalau kaunti 24. Hivyo basi ukiwa mgombea wa kiti chochote cha kisiasa kipindi kijacho, na ulionekana kuunga mkono kupugunzwa kwa pesa kwa kaunti hizi, huenda ukapigwa mijeledi na wapiga kura ; Wapiga kura hao huenda wakasikika wakisema………..

“unamwona huyu anayetaka kura zetu, miaka miwili iliyopita, aliunga mkono mfumo wa kupunguza kitita chetu cha mgao.”

Vilevile kuna Baadhi ya maseneta ambao tayari wamesikika wakisema..
      “Mkipunguza pesa zetu , hata msilete BBI hapa”

Kumbuka kulingana na BBI, ajenda kubwa ni pesa mashinani.

Wacha nikupe Orodha kidogo tu za zile kaunti ambazo zitaongezewa pesa iwapo mfumo huu utaidhinishwa. Kiambu bilioni 1.3, Nairobi bilioni 1.2, Uashin Ghishu milioni 923, Nandi milioni 788 Kajiado milioni 665, Nakuru milioni 744, Laikipia milioni 660 Transzoia milioni  626, Kirinyagga milioni 538, Baringo milioni 537, Bomet milioni 456, West Pokot milioni 444, Kakamega milioni 402, Bungoma milioni 400 , Machakos milioni 367, Embu milioni 356. Kwa hivyo kaunti za Pwani, na kaunti za eno za Kaskazini mashariki,zitapoteza ilhali kaunti za Rift Valley, Western, Nyanza na Central zitaongezewa kwasababu huko kuna wingi wa watu.

Alhamisi maseneta walishindwa kusuluhisha swala hilo,  hivi sasa lazima wakutane tena upesi, kikao ambacho tayari kimepangwa kesho Jumanne tarehe 28 Julai walisuluhishe kwasababu, hii ndio fomyula ya kuwagawa kaunti zetu pesa ,kumaanisha , serikali za kaunti kwa sasa haziwezi kujadili bajeti zao wa mwaka huu wa fedha; Mbona? watafanya bajeti cha kiwango kipi cha pesa? Unaweza fanya bajeti, pesa zako zipunguzwe, ama pia ukafanye bajeti ndogo ilhali pesa zako zikaongezwa, na ujue fomyula ambayo itatumika mwaka huu inafaa kutupeleka kwa miaka sita, kwa hivyo kuna mtu anayeingalia kuwa ukitupunguzia leo, inamaanisha kuwa kwa miaka sita, tutakuwa tukipoteza, wakati kuna mwengine anayehisi kuwa kwa mika sita atakuwa akiongezwa.

Ni sawa na kujaribu kumnyanga mtoto pipi mdomoni… si rahisi.

Ukweli mchungu hata hivyo ni kuwa, tusitarajie kuwa maseneta watakubaliana kwa urahisi, ni sawa na kazini, wafanyakazi waambiwe kuwa wakae chini wakaamue nani apunguziwe mshahara ili mwengine anufaike eti kwa sababu kwake ana watoto wengi ama kwa sababu wewe bado kapera huhitaji hela nyingi, hivyo mshahara wako ukapunguzwe ili mwenzako iliyeoa juzi akapata zaidi. si rahisi.

Pendekezo langu kama mwana Uchumi mwenye tajriba ya uchumu wa nchi,

Jukumu hili lingeachiwa C.R.A. Commission on Revenue Allocation, najua , ni wajibu wa maseneta na ni miongoni mwa majukumu yao, lakini pia michango ya wenye tajriba pana ya uchumi, michango ya watu ambao wanaweza kukalia chini fomyula hii na ikaamuliwa barabara pasi na siasa zozote ambazo tumeanza kushuhudia, za kujipenda, handshake na uchaguzi ujao wa 2022.

Ukiniuliza, kigezo kikuu ambacho tungekuwa tunazungumzia hapa, ni poverty index , ni sehemu zipi ambazo zimesalia nyuma saana kimaendeleo, ili ugatuzi isiwe kisingizio cha kuyeyusha sehemu zingine ambazo tayari zimefilisika kutokana na kudorora kwa uchumi Hata kama tutazungumzia asilimia 15 ambazo zitafikia kaunti hizi kwa usawa ni sawa, lakini tungalia ni sehemu zipi zinategemea ugatuzi kwa asilimia kubwa, ili kuhakikisha kwamba wakaazi wake ambao hawajapata masomo, ama wakazi au akina mama ambao hawajawahi kujifungulia kwa hospitali kutokana na umaskini, angalau wameinuka kutokana na ugatuzi na kusaidika zaidi.

                                                                             Mwandishi, @Odhiambo, ana uzoefu na tajriba katika maswala ya Uchumi wa kitaifa.
https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287