Harakati za mwisho kwa safari za ndege.

Mashirika ya ndege za Kimataifa yametangaza rasmi kurejelea safari zao za ndege humu nchini.
Kulingana na taarifa zilizotumwa kwa meza yetu ya uchumi na biashara, wanaopanga kusafiri kuenda nje ya nchi wanafaa kuanza kujitayarisha kurejelea safari za ndege za kimataifa kuanzia tarehe mosi mwezi ujao.
Shirika la ndege la British airways kwa mfano, limesema litakuwa na safari nne za ndege kwa wiki, kuja na kutoka Nairobi siku ya Jumanne, Alhamisi , Jumamosi na Jumapili,wakati shirika la Ndege la France likitangaza safari moja ya kila siku ya Ijumaa kuelekea mjini Paris.
Ndege la shirika la Qatar limesema kuwa litaanza safari zake tarehe 3 mweziAgosti huku shirika la Emirates likisema kuwa liko tayarikurejelea safari zake tarehe 28 mwezi huu kuwaondoa abiria humu nchini kuwapeleka kule Dubai.
Mashirika yote yamewataka wateja wao kuzingatia maagizo yanayotolewa na serikali wakati wa safari hizo.
Yakijiri haya, marubani na wafanyakazi wa ndege za kimataifa hawataruhusiwa kuondoka katika hoteli zao au vyumba vyao vya kulala ila tu kukiwa na dharura.
Masharti makali za kiafya zilizochapishwa na Wizara ya Utalii kwa kushirikiana na ile ya Afya zinaonyesha kuwa mlo na vinywaji vya hoteli vitakavyotengwa kwa marubani na wafanyakazi hao wa ndege pekee ndizo zitaruhusiwa kutumika bila kuagiza chochote nje.
Shirika la KQ, ilifikia makubaliano na serikali ambayo itaona wafanyakazi wake wanaporudi nchini kutoka safari za nje ya nchi hawalazimishwi kwa karantini ya lazima.