Chama tawala Tanzania, CCM kuanzisha mchujo kwa wagombea wake kipitia kura ya maoni

UK election: More than 620,000 beat midnight deadline to apply for ...Chama tawala nchini Tanzania CCM kimeanza mchakato wa kuwachuja wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani kupitia kura za maoni zinazofanyika kote nchini.

Wagombea wa nafasi zote wanajinadi kwa wapiga kura hatimaye kuamua hatma yao kutokana na matokeo yanayotarajiwa.

Aidha kutokana na wingi  wa wagombea waliojitokeza kuwania nafasi za kuchaguliwa huwenda Kura hizi za maoni zikawa moja ya mtihani mkubwa katika chama hicho , jambo linadhihirika kwa uwazi.

Mbali na wabunge waliomaliza muda wao kurejea tena kwenye kinyang’anyiro hicho, wateule wa rais ikiwemo wakuu wa mikoa,wilaya na makatibu wakuu nao pia wamo kwenye mbio hizo.

hatahivyo leo na kesho Jumanne zitakuwa siku muhimu kwa chama hicho kinapoanza hatua za mwanzo kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

https://bouhoagy.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287