Mkaazi wa Mombasa avunja rekodi ya mapishi duniani

By Yussuf Abubakar
Mpishi mkenya kutoka kauti ya Mombasa Maliha Mohammed, ameandikisha historia kwa kuvunja rekodi ya mapishi duniani kwa kupika saa 75 mfululizo.
Maliha alivunja rekodi iliyowekwa na mmarekani Rickie Lamkin ya saa 68 disemba mwaka jana.Maliha alianza zoezi hilo siku ya alhamisi na kufikia jana jumapili mwendo wa saa saba akawa amekamilisha saa 75.
Waliokuwa wakimsaidia kufanikisha ndoto yake vilevile walifurahia ushindi huo wakiwemo familia pamoja na wakaazi.
Kwa sasa Maliha anasubiri maamuzi kutoka kwa maafisa wa kitabu cha kumbukumbu duniani cha Guiness kutoka uengereza.