Manchester United,Porto zasonga mbele

Timu ya Manchester United imefuzu kwenye hatua ya robo fainali ya kombe la klabu bingwa barani ulaya hii ni baada ya kuilaza timu ya PSG mabao 3-1 kwenye mechi ya mkondo wa pili iliyochezwa katika uwanja wa Perc des Princes huko nchini Ufaransa.

United walitangulia kufunga kunako dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku kisha akaongeza la pili dakika ya 30 naye mshambuliaji Murcus Rashford akafunga la tatu kwenye dakika ya 90 ya mchezo kupitia kwa mkwaju wa penalti.Bao la kufutia machozi la PSG lilifungwa na Juan Bernat kunako dakika ya 12.

Kwa ujumla timu ya Man United imefunzu kutokana na mabao mengi ya ugenini licha ya kutoka sare ya  mabao 3-3 hii ni baada ya kulazwa mabao 2-0 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.

Na katika matokeo mengine timu ya Porto ya kutoka Ureno imefuzu kwenye hatua hiyo ya robo fainali baada ya kuilaza timu ya Roma  ya kutoka nchini Italia mabao 3-1.Kwa ujumla timu ya Porto imefuzu kwa jumla ya mabao 4-3 hii ni baada ya kupoteza mabao 2-1 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezwa huko Italia.