Jinsi ya kupika supu ya brokoli

Na Mishi Haruni

Supu ya brokoli .

Vipimo

Brokoli – 1 msongo (bunch)
Parlsely – 3 misongo
Karoti – 2
Viazi – 2
Vitunguu – 1 – 2
Nyanya – 1
Kidonge cha supu (stock/ Maggi cube) – 1
Pilipili manga – 1 kijiko cha chai
Chumvi – kiasi
Ndimu – 1 kijiko cha chai
Mafuta – 2 kijiko cha supu
Zaytuni – kiasi

Namna ya kutayarisha na kupika
1. Chambua brokoli, katakata karoti, viazi, vitunguu na nyanya.
2. Chemsha brokoli, karoti na viazi.
3. Tia mafuta katika sufuria kaanga vitunguu hadi vilainike, tia nyanya, endelea kukaanga.
4. Tia pilipilimanga, chumvi na kidonge cha supu.
5. Mimina vitu ulivyochemsha na supu yake katika mkaango.
6. Tia katika mashine ya kusagia (blender).
7. Tia parselye usage kidogo tu, kisha rudisha katika sufuria urejeshe katika moto na ipike kidogo kwa muda wa 1 tu.
8. Onja chumvi, ndimu ikiwa tayari kuliwa pekee au na mkate na zaytuni.

Kwa hisani ya  ALHIDAAYA.COM

https://bouhoagy.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287