Keki ya mchanganyiko wa matunda

Na Mishi Harun

Keki yenye mchanganyiko wa matunda

Vipimo

Unga – 2 Vikombe Mayai – 6
Siagi – 200g
Sukari – 1 Kikombe
Vanilla – ½ Kijiko
Arki rose ukipenda – 2 matone
Baking powder – 2 Vijiko vya chai
Mchanganyiko wa matunda kavu- ¾ Kikombe

Namna ya kutayarisha na kupika

1. Washa oveni 350°c.
2. Saga siagi na sukari kwa mashine mpaka mchanganyiko ulainike.
3. Ongeza yai moja baada ya moja na huku ukiendelea kusaga mpaka yaishe.
4. Tia unga uliochanganwa na baking powder.
5. Endelea kuchanganya mpaka ichanganyike vizuri, halafu arki rose, vanilla na mchnganyiko wa matunda kavu halafu koroga kidogo ilizichanganyike vizuri.
6. Mimina mchanganyiko katika chombo cha kuchomea.
7. Vumbika (bake) kwa muda wa dakika 20 mpaka 25.
8. Ikisha poa kata kata vipande na tayari kuliwa kwa kahawa au chai.

Kwa hisani ya alhidaaya.com

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287