Wali wa Kabsa

Mahitaji

• Mchele 1 1\2 kikombe
• Kuku 600g aliyekatwa katwa vipande vikubwa vikubwa
• Mafuta 1 kikombe
• Vitunguu 2 maji katakata
• Tomato za madonge 5 Zilizokatwa katwa
• Tomato ya mkebe – kijiko 1
• Karoti mbili zilizogretiwa
• Tangawizi mbichi iliyosagwa – kijiko 1\2
• Maganda ya Chungwa iliyosagwa nusu kijiko
• Ndimu iliyokaushwa
• Chumvi kiasi
• Pilipili manga nusu kijiko
• Iliki iliyosagwa nusu kijiko
• Mdalasini iliyosagwa nusu kijiko
• Karafuu iliyosagwa kijiko 1 na robo
• Njugu za Lozi (Almond nuts)
• Zabibu kiasi

Namna ya kutayarisha

Tayarisha sufuria yako iliyosafi na uibandike kwenye moto wa kiasi,mimina mafuta ya uto na uhakikishe yamepata moto na baadae , tia vitunguu maji vilivyokatwakatwa na tangawizi iliyosagwa na uanze kukoroga hadi vibadilike rangi ya dhahabu , mimina maganda ya machungwa yaliyosagwa , pilipili manga, iliki, ndimu, mdalasini,na karafuu katika mchanganyiko huo kisha weka tomato ya mkebe na uendelee kukoroga na baadae ufinike kutumia mfiniko ili tomato zipate kuvurujika na ziive.

Muoshe kuku wako uliyemkatakata vizuri kisha umtumbukize kwenye viungo vyako ulivyovikaanga ,koroga kwa dakika tatu tu kisha mimina maji lita moja kwenye mchanganyiko huo na kumuacha kuku wako aive kwa dakika kumi na tano.

Mtoe kuku wako kwenye ule mchuzi kwa kutumia kijiko ,panga vipande vya kuku kwenye oven na uhakikishe moto utakao utumia ni wa kiasi , osha mchele vizuri na uumwage maji, na badae mimina kwenye ule mchuzi na ukoroge. chukua kareti zilizogretiwa na umimine pia, ukiwa bado unakoroga angalia kiini cha wali na hakikisha umeiva . finika wali wako kwa mfiniko na upunguze moto kwa kiasi ili upishi wako upate kuiva.

Bandika mafuta kwenye karai lako na yakipata moto mimina lozi zako ulizozishambua huku ukikoroga hadi ziwe kavu kabla ya kuepua mafuta chukua zabibu pia uzikaange na baadae uzitoe na uziache zipoe .

Upishi wa kabsa utakua umekamilika na tayari kupakua , baadae utaongezea lozi na zabibu kwa juu pamoja na kuku wako baada ya kumtoa kwenye oven .

https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287