Jinsi ya kuandaa uji wa kunde

Mahitaji na vipimo vyake


• Kunde Kavu – 2 Vikombe
• Tui – 1 Kikombe
• Sukari – 1 Kikombe
• Maji – 7 Vikombe
• Garam masala – ½ Kijiko cha chai
• Hiliki – Kiasi
• Karafuu – 3-4 Chembe
• Pilipili manga – ½ Kijiko cha chai
• Chumvi – Chembe kidogo

Namna ya kutayarisha na kupika
1. Chemsha kunde kavu bila yakuroweka kwa maji vikombe 4 na sukari kikombe kimoja kwa moto kiasi mpaka ziwive
2. Kisha mimina vitu vyote vilivyobakia pamoja na maji vikombe 3 vilivyobaki na acha ichemke taratibu mpaka maji yapunguke uji uwe mzito.
3. Epua mimina kwenye bakuli ukiwa tayari

Kwa hisani ya ALHIDAAYA.COM

https://ptauxofi.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287