Mahakama ya Mombasa yatoa agizo

Viongozi wakiwa katika mahakama kuu ya Mombasa wakifuatilia kesi ya kijana aliyepotea/Photo na Munna Swalleh.

Jaji wa mahakama ya Mombasa Erick Ogolla ametoa agizo la kuwasilishwa mbele ya mahakama Husni Mbaraq aliyekuwa amepotea kwa mda wa mwezi mmoja itakapofikia Juni 29.
Mahakama imeelezwa kuwa Husni Mbaraq alikuwa ametoka mskitini kuswali swala ya ijumaa mnamo Mei 25 na hatimaye kuchukuliwa na watu wasiojulikana.
Aidha mbunge wa kaunti ya Mombasa Abduswamad Shariff Nassir amesema kuwa kila mwananchi yuko na uhuru wa kuishi na endapo mtu atapotea bila ya kuonekana basi maafisa wa polisi wachukue hatua na kufanya kazi zao.
Wazazi pamoja na familia ya Husni Mbaraq wametoa malalamishi mbele ya mahakama na kusema kuwa ingawa mtoto wao atakuwa amefanya kosa lolote basi angefikishwa mbele ya mahakama lakini sio kumpoteza.