Kuku wa kufukiza

f

MAHITAJI
• Kuku 1 wa kiasi mkate muoshe
• Kotmir/dania 1
• Tomato ya mkebe vijiko 2
• Vitunguu maji 2
• Kitunguu saum na tangawizi iliyopondwa vijiko 2
• Jira/bizari iliyopondwa kijiko kidogo
• Nyanya zilizoiva 3
• Limau moja
• Maziwa ya mtindi nusu kikombe
• Garam masala kidogo
Namna ya kutayarisha

Weka vitu vyote katika blenda isipokua kuku saga mpaka iwe rojo zito alafu pakaza katika kuku uliomchanja hakikisha kuku unamtoa ngozi kisha weka katika sufutia na kibakuli kipana wekea mafuta ya kupikia kisha tumbukiza makaa ya moto haraka haraka funika na hakikisha mfuniko wako haupenyezi moshi nje.

Sasa bandika moto wa juu na chini wa kiasi mfano wa kuoka, wacha kuku aive na huku kibakuli kinatoa moshi ndani.
Baada ya dakika 40 hadi 50 angalia kama kuku ameiva, iwapo tayari mtowe mwache apoe kidogo.
Andaa kwa Mikati, Wali au Sembe.

https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287