Vijana 10,000 kukongamana Machakos

Zaidi ya wajumbe 10,000 wanatarajiwa kuhudhuria kongamano la vijana kaunti ya Machakos litakaloongozwa na Gavana Alfred Mutua mapema leo hii.
Wajumbe hao kutoka mikoa ya Nyanza, Magharibi, Pwani, Bonde la ufa na Kaskazini mashariki mwa Kenya wameanza kuwasili katika ukumbi wa Machakos kwa ajili ya kongamano hilo.
Gavana wa Machakos Alfred Mutua amesema kuwa uzinduzi huo utaangazia sana suala la “Maendeleo Chap Chap” ambalo lengo lake ni kuinua maslahi ya vijana na wananchi kwa jumla.