Bunge kutoa uamuzi wa mkopo wa bandari ya Mombasa mwezi juni.

htht

Uamuzi wa kutolewa kwa mkopo wa bilioni 27.3 wa mradi wa awamu ya pili ya upanuzi wa bandari ya Mombasa utatolewa mwezi ujao.

Hatua hiyo inafuatia msukumo kutoka kwa wabunge kutaka bunge kusitisha mjadala huo ili kutoa nafasi kwa kamati ya bunge kuhusu fedha, biashara na mipango kuanza kuchunguza mkopo huo.

Wakiongozwa na mbunge wa Suna mashariki, Junet Mohamed, wabunge walitaka mswada huo kusimamishwa kwa muda hadi watakaporudi kwenye vikao vyao mwezi ujao akisema kuwa itatoa nafasi kwa wataoji zabuni kuchunguza ili kuhakikisha kunautumizi mzuri wa mapato yatakayotokana na mradi huo.

Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu fedha, mipango na biashara Benjamin Langat  na kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa AdenNduale wamesisitiza haja ya kujadiliwa kwa mswada huo mwezi ujao baada ya kamati hiyo kutayarisha ripoti ya mkopo huo na kuwasilisha tena bungeni.

Mkopo huo ambao unajadiliwa kwa riba ya asilimia 0.11 kila mwaka utalipwa kwa awamu thelathini na nne kwa kipindi cha miaka sita.

 

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287