Biashara ya pembe za Ndovu yazua mgawanyiko afrika huku kongamano la UN kuhusu biashara likikaribia.

ivory

Mataifa wanachama wa muungano wa kimataifa kuhusu biashara huenda yakawa hayatakutana mwezi septemba kama ilivyodesturi kutokana na baadhi ya mataifa hayo kujitoa kwenye mashindano hayo kufuatia mgawanyiko unaochangiwa na biashara ya pembe za ndovu.

Mapendekezo ya kongamano hilo litakaloandaliwa mjini Johannesburg nchini Afrika kusini yaliwekwa wazi wiki hii huku Namibia na Zimbabwe yakitarajiwa kufungua kongamano hilo kwa biashara ya pembe za ndovu kinyume na taifa la kenya na mataifa mengine duniani yanayopinga biashara hiyo.

Aidha mataifa yanayopinga biashara hiyo yanasema kuwa ikiwa bidhaa zinazotokana na wanyama pori zitaruhusiwa basi huenda ikawa pigo kwa mataifa hayo kwani itawalazimu kutumia fedha nyingi zaidi katika kuwatunza wanyama hao.

Hata hivyo katibu mkuu wa muungano huo JohnScanlon amesema mataifa changamoto kuu inayowakumba ni iwapo wanyama hawa watasalia katika mbuga zao ikiwa biashara hiyo itahalalishwa kote duniani.

 

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287