Grilled Chicken

Mahitaji
Kuku 1
Maembe mabichi 5
Tumeric vijiko 5
Spices kiasi
Chumvi 22gms
Mafuta 15gms
Pilipili Manga 3gms
Paprika 60gms
Kitunguu saumu 15gms

Namna ya Kutayarisha
Anza kwa kutengeza Amba Sauce.
Hii unachambua maganda ya maembe mabichi kisha unayaroweka na chumvi kwa siku mbili hadi nne.
Baada ya kuyaroweka utayamimina kwenye blender uongeze tumeric na spices usage hadi yasagike vizuri.
Hapo Amba Sauce yako itakuwa tayari.

Sasa unatayarisha chicken wing sauce

Sasa chukua bakuli safi upime 90gms za amba sauce,paprika 60gms,chumvi 22gms,mafuta 300gms,pilipili manga 3gms,kitunguu saumu 15gms
Changanya vyote vizuri.
Alafu msafishe kuku wako umkate vipande vinne.
Kisha mtie kwenye chicken wing sauce uhakikishe kuwa pande zote zimeingia sauce vizuri.
Hakikisha kuwa jiko lako liko tayari na makaa yameshika moto vizuri.
Mchome kuku wako huku ukijeuza jeuza hadi aive.
Unaweza kula kwa chips,wali au chochote upendacho.
Nakutakia uandazi mwema.

https://uwoaptee.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287