Barafu za custard

Mahitaji
Maziwa vikombe 3
Sukari 1/2 kikombe
Vijiko 2 custard changanya na vijiko 5 vya maji.

Namna ya kutayarisha
Katika sufuria tia maziwa na sukari kisha ubandike kwenye jiko ichemke.
Ikishaanza kuchemka tia custard na maji ukoroge vizuri.
Vikishachanganyika epua.
Kama mchanganyiko huo bado ni mzito ongeza maziwa na maji uchanganye hadi upate uzito unaotaka.
Alafu mimina mchanganyiko kwenye chombo,vikombe unaweza kutia na vijiti.
Sasa weka kwenye freezer hadi zishike donge.
Nakutakia uandazi mwema.

https://upskittyan.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287