Chauro
Dengu 1/2 Kilo
Njugu zilizo kaangwa ¼ kilo
Korosho ¼ Kilo
Viazi kiasi
Bizari ya manjano kijiko 1
Sukari ¼ kikombe
Chumvi Kiasi
Ndimu ya unga vijiko 2
Majani ya bajia kiasi
Mafuta kiasi
Namna Ya Kutayarisha
Roweka dengu tokea usiku.
Siku ya pili weka mafuta kwenye karai,umoto wa kiasi kaanga dengu kisha uzitoe.
Alafu toa viazi maganda,uvioshe kisha uvikate slices na uvikaange kama kachiri.
Sasa tia mafuta vijiko 2 katika kikaango ukaange majani ya mchuzi pamoja na bizari ya manjano.
Tia kwenye bakuli kubwa vitu vyote ulivyokaanga na uchanganye , pamoja na korosho na njugu
Nyunyuzia sukari, ndimu ya unga, chumvi uchanganye vyote pamoja tayari kuliwa.
Nakutakia uandazi mwema.