"> IDADI YA WATALII YATARAJIWA KUONGEZEKA. – Salaam Fm

IDADI YA WATALII YATARAJIWA KUONGEZEKA.

 
TTIdadi  ya watalii wanaozuru humu nchini inatarajwia kuongezeka huku sherehe za kuadhimisha miaka 100 tangu  vita vya dunia vya kwanza kutokea.
 
Gavana wa kaunti ya Taita Taveta John Mruttu amesema kuwa sekta ya utalii  itaweza kuimarika na  kuendeleza uchumi wa Kenya.
 
Wakati huo huo Mruttu ameongeza kuwa  anatarajia idadi kubwa ya watalii   hao kuzuru kaunti ya Taita  Taveta kutokana na maadhimisho hayo.
 
Mruttu ameongeza kuwa wamebuni  mikakati  ya maendeleo itakayoimarisha sekta ya utalii katika kaunti hiyo.
 
 
NA Ibtisam Jamal.