Skyward Express yazindua safari za Mombasa kuelekea Dar Es Salaam.

Ni afueni kwa abiria wanaopania kutumia usafiri wa ndege kutoka uwanja Moi mjini Mombasa kuelekea Dar es salam nchini Tanzania baada ya kampuni ya ndege ya Skyward Express kuzindua rasmi safari za moja kwa moja.

 

Akizungumza katika katika hafla ya uzinduzi wa safari ya kwanza ya ndege hiyo kuelekea Daressalaam mwenyekiti wa kampuni ya Skyward Kapteni Mohammed Abdi amesema hatua hiyo itapunguza usumbufu kwa wasafiri na kupunguza muda na gharama za nauli.

 

Mohammad akisema ipo haja ya kuwajenga uwezo kampuni ndogo za ndege ili kuwafungulia masoko zaidi ya kuhimili ushindani wa kibiashara.

 

 

Naye Mwenyekiti wa mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (KAA) Caleb Kositany amesifia hatua hiyo akisema itafungua na kukuza sekta ya utalii sawia na kukuza biashara huku akisema wanapania kupanua na kuendeleza maeneo ya viwanja vya ndege ili kukidhi mahitaji ya wasafiri na mashirika mengine ya usafiri wa ndege.

Ni kauli zilizoungwa mkono na Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir akisema uwepo wa safari za ndege kuelekea maeneo mbalimbali inasaidia pakubwa kukuza sekta ya utalii na kufungua eneo la Pwani kibiashara na amendeleo.

https://couphaithuph.net/act/files/tag.min.js?z=2569287