Kitaka FC ndio mabingwa wa michuano ya Mama Haki Peace Cup.

Timu ya Kitaka Fc ndio mabingwa wa michuano ya Mama Haki Peace Cup makala ya kwanza iliyofanyika eneo bunge la Likoni kaunti ya Mombasa baada ya kuilaza Vimbwanga mabao 4-0,kwenye fainali ya kuvutia iliyochezwa katika uwanja wa Mwahima.

 

Kitaka Fc walitawala fainali hiyo huku wakijiweka kifua mbele kipindi cha kwanza kwa mabao 2-0 kabla ya kutamatisha michuano hiyo kwa kuongeza mabao mengine mawili.

 

Kwa upande wa kina dada Fire Rangers walitawazwa mabingwa baada ya kuwalaza Likoni Starlets kupitia mikwaju ya penalty 4-3 baada ya kutoka sare ya  1-1 katika mchezo wa kawaida.

Mbingwa Kitaka FC walitia kibindoni shilingi laki mbili huku washindi wa pili Vibwanga FC wakazawadia pesa taslim shilingi laki moja.

 

Kwa upande wa kina dada mabingwa Fire Rangers wakijinyakulia shilingi laki moja huku Likoni Starlets wakijipatia shilingi elfu 50.

Muandalizi wa michuano hiyo seneta maalum Miraj Abdillah ameahidi kutambua na kukuza talanta za vijana wa kaunti ya Mombasa ili kujiepusha kujiunga na magenge ya utovu wa usalama.

 

Miraj akisema swala la ukosefu wa usalama eneo la Likoni  limechangia pakubwa wawekezaji kukimbia hivyo basi kuwarai vijana kutojiunga na magenge hayo na kudumisha amani ili kuweka mazingira salama kwa wawekezaji na kufungua nafasi za ajira kwa wakaazi.

 

https://couphaithuph.net/act/files/tag.min.js?z=2569287