Wanafunzi 300 eneo bunge la Jomvu wafaidika na ufadhili wa masomo kutoka kwa wakfu wa Karisa Nzai.

Jumla ya wanafunzi 300 kutoka eneo bunge la Jomvu  wamefaidika na ufadhili wa masomo kutoka Kwa wakfu wa Karisa Nzai.

Ufadhili huo ambao uko chini ya udhamini wa mshauri wa rais Wiliam Ruto katika maswala ya siasa Muheshimiwa Karisa Nzai utawafaidi wanafunzi wa shule ya upili,vyuo vya kadri pamoja na vyuo vikuu.

Akiongeaa wakati wa hafla ya kuwakabidhi hundi za fedha wazazi katika eneo la mikindani eneo bunge la Jomvu,Nzai amesema azma yake ya kuanzisha ufadhili huo imetokana na changamoto za maisha ambazo wazazi wanapitia kuwafundisha watoto wao licha ya kuwepo Kwa fedha maalum kutoka Kwa  serikali ambazo wametengewa wanafunzi.

Nzai akisema mpango huo endelevu utawafaidi wanafunzi wanapoanza masomo hadi kumaliza.

 

Aidha Nzai amesema Kuna mfumo maalum ambao unazingatiwa katika kupeana ufadhili huo huku wale wasio na uwezo na mayatima wakipewa kipaumbele.

 

 

Kwa upande wao wazazi ambao watoto wao wamefaidika na ufadhili huo wamemshkuru Karisa Nzai Kwa  ufadhili huo wakisema utawafaidi pakubwa na kuenua kiwango cha elimu katika eneo bunge la Jomvu pamoja na kupunguza kero la wanafunzi kutumwa nyumbani mara Kwa mara sababu ya ada.

 

https://kukrosti.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287