Viongozi wa Azimio Mombasa watakiwa kusitisha Maandamano dhidi ya serikali
VIONGOZI wa chama cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa wamewatahadharisha wenzao wa mrengo wa azimio la Umoja dhidi ya kushinikiza na kuongoza maandamano ya kila wiki ya kupinga serikali kwenye kaunti hiyo.
Wakiongozwa na Naibu mwenyekiti wa chama cha UDA ambaye pia ni Mbunge wa Afrika wa Afrika Mashariki Hassan Omar Sarai Viongozi hao wameendelea kuyashutumu maandamano hayo ya upinzani wakiyataja kuwa yenye nia ya kuhujumu miradi ya maendeleo inayoendekezwa na serikali ya Kenya Kwanza.
Kulingana na Sarai Mrengo wa upinzani hauna sababu ya msingi ya kuandaa maadamano hayo hivyo Amesema endapo kutazuka ghasia na uharibifu wa Mali wakati wa maandamano hayo ni sharti viongozi hao wanaohusika kuwajibishwa ipasavyo kisheria.
Wakati huo huo ameendelea kuwarai Viongozi hao wa mrengo wa upinzani kwenye kaunti hiyo kusitisha maandamano na kuungana na serikali kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wakaazi.
Mbali na hayo Sarai amemshukuru rais William Ruto kwa kuteua wapwani kuhudumu katika idara na taasisi mbalimbali za serikali sawia na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo hilo kama alivyoahidi wakati wa kampeni.
Kwa upande wake Charles Kanyi Nyanjua kwa jina maarufu Jaguar ambaye ni waziri msaidizi mteule katika wizara Michezo vijana na sanaa, ametaka vijana kote nchini kuepuka kuchochewa na wanasiasa ili kushiriki maandamano hayo.
Nyagua wakati huo huo ametaka kinara wa mrengo wa Azimio la Umoja Raila Odinga kusitisha maandamano ya kila wiki ili kutoa fursa kwa uongozi uliyomamlakani chini ya Rais William Samoei Ruto kutimiza ahadi ilizoziweka kwa wakenya.