Kampuni ya Isuzu EA kushirikiana na chuo cha KNCP kukuza wanafunzi
NA ELNORA MWAZO
Kampuni ya utengenezaji magari ya Isuzu EA na chuo cha kiufundi cha Kenya Coast national Polytechnic wameingia Katika makubaliano yanayolenga kuwakuza kitaaluma wanafunzi wanaosomea kozi ya uhandisi wa magari chuoni humo.
Kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Rita Kavashe
makubaliano hayo yananuia kutoa fursa Kwa wanafunzi kupata masomo bora yanayoendana na teknolojia ya kisasa Katika nyanja hiyo sawia na kuboresha mtaala unaofundishwa chuoni humo
Aidha amedokeza kuwa kupitia mpango huo wanafunzi hao watapa fursa ya kuendeleza masomo Yao ya nyanjani Katika kampuni ya Isuzu na pia kutafutiwa nafasi za ajira watakapokamilisha masomo Yao.
Hatahivyo akizungumza Wakati wa hafla ya kutiwa sahihi makubaliano hayo Mwalimu mkuu wa chuo hicho Mary Muthoka ameonyesha furaha yake kufuatia ushirikiano huo akisema utachangia pakubwa kukuza maarifa ya utumizi wa teknolojia miongoni mwa wanafunzi wa kozi hiyo.
Kwa upande wake waziri wa elimu Katika serikali ya Kaunti ya Mombasa Daktari Mbwanaali Kame amedokeza kuwa serikali ya Kaunti ya Mombasa inanuia kuanzisha uhamasisho miongoni mwa wanafunzi ambao hawakufanya vyema Katika mtihani wa kitaifa wa KCSE kujiunga na vyuo vya kiufundi.
Amesema serikali ya Kaunti ya Mombasa hivi karibuni itabuni Sera itakayohakikisha kuwa wanafunzi watakaojiunga na vyuo hivyo watapata basari ili kuwawezesha kuendeleza masomo Yao kikamilifu.