Seneta mteule Miraj Abdillah awahimiza wananchi kupanda miti kukabili mabadiliko ya tabia nchi.

Huku serikali ya Kenya ikiendelea na haraki ya upanzi wa miti bilioni tano ndani ya mwaka mmoja kama njia moja ya kukabiliana na tabia nchi,seneta mteule kutoka Mombasa Miraj Abdilah amendleza harakati hizo katika ukanda wa pwani kwa kupanda miti elfu mbili katika shule ya msingi ya mwangala na mtongwe.

Akiongea na wanahabari katika shule ya msingi ya mwangala seneta Miraj ameyataka mashirika ya kimataifa kushirikiana na wanajamii ili kuwahimiza kupanda miti kama njia moja wapo ya kukabiliana na tabia nchi sawia na kuwaelimisha umuhimu wa kutumnza mazingira.

Miraj akisema ananuwia kupanda miti milioni moja katika ukanda wa pwani huku akiahidi kushirikiana na viongozi mbalimbali kufaulisha harakati hizo.

Aidha miraj amewarai wananchi kutumia njia ya kuhifadhi maji wakati wa mvua haswa katika maeneo kame ili  kuyatumia baadae kuimarisha mazingira.

Miraj amesema serikali ya raisi William Ruto ina mikakati maalum kupitia hazina ya hastla kuwaajiri vijana ambao watakuwa waangalizi wa miti hiyo ili kuwa na mazingira bora.


Kwa upande wake kaunti kamishana wa kaunti ya Mombasa John Otieno amewahimiza wananchi kupanda miti kama njia moja wapo ya kukabiliana na tabia nchi haswa katika maeneo kame.

https://bouhoagy.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287