Maadhimisho ya Siku 16 Dhidi ya dhulma za kijinsia yaanza rasmi

NA FATHMA RAJAB

Serikali ya kaunti ya Mombasa Kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii imeandaa matembezi ya kuzindua maadhimisho ya siku 16 dhidi ya dhulma za kijinsia yanayonuia kuweka uhamisho wa kukabiliana na dhulma hizo katika jamii.

Katika kipindi cha Siku kumi na sita hizo Mashirika hayo pamoja na Serikali kuu na zile za Kaunti yanatarajiwa kuungana pamoja na kuendeleza uhamasisho ili kumaliza visa vya  dhulma hizo katika jamii.

Miongoni mwa Shirika lililo mstari katika maadhimisho ya siku hizo  ni  Shirika la Kutoa misaada la Marekani USAID Chini ya Mradi wa  USAID Jitegemee ambao unajihusisha na  kuwasaidia watoto wa kike kujimudu na kujiwezesha kifedha kama njia mojawapo yakuwalinda  dhidi ya dhulma za kijinsia.

Akiongea na wanahabari katika hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku hizo katika Kaunti ya Mombasa, afisa wa jinsia wa jinsia wa Kaunti hiyo kutoka Serikali kuu Meali Hassan amewataka akina mama na wasichana kupiga ripoti haraka endapo watadhulumiwa kingono ili hatua muafaka za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya watekelezaji wa dhulma hizo.

Aidha ametaja umasikini na utumizi wa Mihadarati kuwa sababu kuu zinazochangia kuonzeka Kwa visa hivyo katika Kaunti ya Mombasa,akiyataja maeneo Bunge ya Likoni na Kisauni kuwa yanoyoongoza Kwa visa vya dhulma za kijinsia katika Kaunti hiyo.

Wakati huo huo amewatahadharisha wanajamii dhidi ya kusuluhisha visa vya dhulma za kijinsia ki nyumbani na badala yake amewahimiza kutafuta Huduma za kisheria ili kuwawezesha wahanga wa visa hivyo kupata Haki ipasavyo.

Kwa upande wake mwakilishi wadi wa eneo Tudor Samir Bhalo ambaye alihudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho hayo ametaja tatizo la msongo wa mawazo kutokana na umasikini kama sababu kuu inayochangia kuongezeka Kwa dhulma hizo nchini, akiishinikiza Serikali kubuni nafasi za ajira zaidi ili kukabiliana na tatizo Hilo.

 

Wakati huo huo ameirai idara ya mahakama kuhakikisha kuwa ina harakisha mchakato wa kusikiliza na kuamua kesi zinazohusiana na dhulma za kijinsia dhidi ya watoto na akina mama.

 

 

 

 

 

https://kukrosti.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287