Jamii ya Wanaoishi na ulemavu Mombasa yataka Serikali kuwawekea miundomsingi inayowakidhi

FATMA RAJAB:
Jamii ya watu wanaoishi na ulemavu kaunti ya Mombasa wameitaka serikali ya kaunti hio kuboresha ofisi zake za kiserikali Ili kuwarahisishia wao kupata huduma pindi wanapohitaji.
Mwenyekiti wa jamii ya watu hao Charity Chahasi ameeleza kuwa nyingi ya afisi hizo hazina lift zinazowawezesha kupanda juu ili kupata huduma za kiserikali ivo basi kuwabagua wanaoishi na ulemavu nakuitaka serikali kuhakikisha afisi hizo Zina mazingira yalio Bora kwao.
Chahasi pia ameitaka serikali ya kaunti hio kutenga fedha maalum kutoka wizara ya Treasury zitakazosaidia katika kufanyia marekebisho ofisi hizo
Aidha mashirika ya kutetea haki za binadamu wameipa makataa ya siku 10 yakujadiliana mbinu zakuboresha afisi zote za kiserikali la sivyo kuandaa migomo sawia nakuelekea mahakamani ili kuhakikisha haki dhidi ya jamii hio inapatikana