Ruto aapa kukabiliana na walanguzi wa mihadarati nchini

Siku chache tu baada ya Seneta Mteule kupitia chama cha UDA Miraj Abdillahi kumrai rais William Ruto Kutekeleza ahadi aliyoiweka ya kukabiliana na tatizo la ulanguzi wa dawa za kulevya Nchini ili kukabiliana na visa vya utovu wa usalama, vita hivyo sasa vinaonekaña kuchukua mkondo mpya baada ya Rais Ruto Kutoa onyo Kali dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya Nchini.

Akizungumza wakati wa ziara yake rasmi katika kanda ya pwani rais Ruto amebainisha kuwa Serikali yake imeweka Mipango kabambe ya kukabiliana na walanguzi wa dawa hizo.

wakati huo huo rais Ruto amesema kuwa kamwe taifa la Kenya halitatutumika na walanguzi wa dawa za kulevya kama sehemu ya kuendeleza kuendeleza biashara hiyo haramu,Akivitaka vitengo vya usalama usalama nchini kuwa ange zaidi ili kuwatia mbaroni walangu hao.

Kauli ya rais Ruto inajiri siku chache tu baada ya Mahojiano ya Seneta Mteule wa chama cha UDA miraji Abdillahi na idhaa moja ya televisheni hapa Nchini ambapo aliutaja utepepevu wa vitengo usalama kukabiliana na tatizo la Mihadarati jambo linalozidisha athari miongoni mwa vijana huku visa vya utovu wa usalama vikiendelea kushuhudiwa.

https://bouhoagy.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287