ICPAK yazitaka Serikali mpya za kaunti kulipa malimbikizi ya Madeni

Mwenyekiti wa kitaifa wa taasisi ya wahasibu nchini ICPAK George Mokua amezitaka serikali za kaunti kutopuulzia mbali suala la ulimbikizaji wa madeni ili kuzuia kuathirika Kwa shughuli za kiserikali.

Taasisi hiyo ya ICPAK inashinikiza serikali za kaunti zilizorithi malimbikizi ya madeni kutoka serikali zilizoondoka kuweka mikakati thabiti kuhakikisha wanalipa madeni bila kuyakwepa.

George Mokua amesema kuwa utaratibu wa kisheria sharti ufuate kudhibitisha ukweli kuhusu madeni hayo kabila ya malipo kufanywa.

Mokua kadhalika amehimiza serikali za kaunti vile vile kutolegezea kamba suala la ukusanyaji ushuru, akihoji kwamba tatizo la upungufu wa ukusanyaji ushuru pia huchangia hali hiyo.

https://eechicha.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287