Kemri yaweka mikakati kukabiliana na Ebola

Taasisi ya Utafiti wa matibabu nchini Kemri imeweka mikakati Muafaka ya kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola endapo utaripotiwa humu nchini.

Miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja Kuendelezwa kwa majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo sawia na kuboresha miundomsingi katika maabara ili kuwawezesha wanasayansi kukagua na kufuatilia ugonjwa huo kikamilifu.

Akizungumza katika maonyesho ya kilimo yanayoendelea katika uwanja wa Mkomani kaunti ya Mombasa, Mwanasayansi wa taasisi hiyo Dakta Sophy Uyoga aidha amedokeza kuwa kuwa taasisi ya Kemri imekuwa mstari mbele kukabiliana na ugonjwa wa saratani ya uzazi kwa kuhakikisha kuwa chanjo ya HPV inatolewa kwa wasichana wanaofaa ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa huo.

Daktari Sophie Uyoga kutoka taasisi ya Kemri akipokea tuzo la onyesho bora katika sehemu ya huduma katika sekta afya na phamasia(dawa) kutoka kwa naibu rais Rigathi Gachagua Wakati wa maonyesho ya kilimo ya Mombasa mwaka 2022.

 

Wakati huo huo ameisifu mikakati ya matumizi ya Teknolojia iliyowekwa na taasisi hiyo wakati wa janga la virusi vya Korona, akisema kuwa iliisadia pakubwa wizara ya afya nchini kutathmini athari zilizoletwa na janga hilo katika jamii.
Aidha amedokeza kuwa kutokana na matumizi ya teknolojia wamefanikiwa kuvumbua vifaa vya kupima magonjwa Korona na Malaria na kuwa wanaendeleza mikakati ya kuidhinisha matumizi yake katika katika mataifa ya nje.

Aidha Dakta Sophy amewahimiza wanafunzi wa shule za msingi na upili kuyapa kipaumbele masomo ya sayansi ili kuwawezesha kuwa katika nafasi bora ya kutatua changamoto za kisayansi zitakazoibuka siku za usoni.

https://boustahe.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287