YWCA yaandaa Kongamano kujadili changamoto za wanawake wadogo

Shirika la Young Women Christian of Kenya Association of Kenya linaanda Kongamano katika Kaunti ya Mombasa linalonuia Kujadili na kutafuta suluhisho Kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake wadogo nchini.

Kongamano Hilo ambalo kauli mbiu yake ni kuwawezesha wanawake wajasiriamali wenye umri mdogo kujikwamua kiuchumi, pia linalenga kuwaepushia wanawake visa vya dhulma za kingono na kijinsia Kwa kujihusisha na shughuli za kibiashara.

Kulingana na afisa wa mipango katika Shirika la YMCA Rebecca Mayabi Kongamano Hilo limetoa fursa Kwa wanawake wajasiriamali kuelezea changamoto mbalimbali zinazowakumba kutokana utumizi wa Teknolojia katika biashara, ambapo wataalamu wanahusishwa katika kujadili na kutoa suluhisho kuhusiana na changamoto hizo.

Wakati huo huo ameonyesha matumaini ya kutekelezwa Kwa mabadiliko ya sera na mapendekezo ya sheria mbalimbali Kwa faida ya wanawake ambazo zimeahidiwa na Viongozi waliyohudhuria Kongamano Hilo,akisema kama Shirika watafutilia Kwa ukaribu ili kuhakikisha kuwa ahadi hizo zinatimizwa.

Wanawake wanaohudhuria Kongamano Hilo kutoka maeneo mengine ya nchini wamewarai Viongozi wa kiasiasa kushirikiana pamoja na kusukuma mbele Sera na sheria za manufaa Kwa manufaa ya wanawake wote nchini.

 

 

https://itweepinbelltor.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287