Serikali kushtakiwa endapo haitawaachilia wakenya waliyopotezwa kimabavu

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Haki Africa Hussein Khalid akihutubia mkutano wa nyuma

Shirika la utetezi wa haki za kibinaadamu la Haki Africa limetishia kuwasilisha kesi ya pamoja mahakamani ili kuishinikiza serikali kuwaachilia wakenya wote waliyopotezwa kupitia njia tatanishi na kitengo cha huduma maalumu SSU kilichovunjwa hivi majuzi.

Kulingana na afisa wa maswala ya dharura katika shirika hilo Mathias Shipeta,katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita wamenakili jumla ya visa 235 vya watu waliyouliwa kiholel na na wengine kupotezwa kwa mabavu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini katika ofisi za shirika hilo wakati alipokutana na familia 20 zilizowapoteza jamaa zao kwa njia tatanishi katika eneo la pwani, Shipeta ametoa makataa ya siku 14 kwa serikali kuwaregesha wakenya hao la sivyo wachukue hatua za kisheria.

Aidha Shipeta amebainisha kuwa ndani ya miaka minne iliyopita ni wakenya thelathini pekee ambao walikuwa wamepotezwa wamefanikiwa kuregeshwa na kuungana tena na familia zao,akiishinikiza serikali kuwaachilia wahanga wengine hasa ikizingatiwa kuwa kitengo kinachoaminika kutekeleza utekaji huo tayari kimebanduliwa.

Wakati huo huo  familia zilipoteza jamaa wao kupitia njia tatanishi, zimeiomba serikali kuingilia kati na   kuwaregesha wakiwa wakiwa wazima huku wakijawa na matumaini ya kuwapata wakiwa  wangali hai.

https://itweepinbelltor.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287