Watu laki mbili wabainika kuathiriwa na ukame Kwale

Kamishina wa kaunti ya kwale Gidion Oyagi ametaja ukosefu wa mvua kwa muda mrefu kuwa sababu iliyochamgia ukame unaoshuhudiwa eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea chakula cha ruzuku kutoka kwa sarikali kuu,Kamishna huyo amebainisha kuwa jumla ya wakaazi laki 2 wamekuwa wahanga wa janga la ukame kaunti ya kwale huku akisistiza kuwa mikakati imewekwa na serikali ya kitaifa na ile ya kaunti hiyo ili kupunguza maafa zaidi.
Oyagi amesema wamepokea chakula cha awamu ya kwanza huku akiongeza kuwa eneo la  samburu linauhitaji wa zaidi msaada huo.

Aidha kamishna huyo amewahakikishia wakazi wa eneo hilo kuwa  chakula hicho kitawafikia wahusika kama ilivyoratibiwa.

Kadhalika kamishna huyo amewataka wakaazi kujitokeza na kuwasaidia kuzitambua familia zilizoathirika moja kwa moja.

https://eechicha.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287