Familia Likoni yaendelea kumtafuta mwanao mwaka mmoja baada ya kupotezwa

Familia moja katika Kaunti ya Mombasa inaiomba Serikali ya kitaifa kuingilia Kati na kumtafuta mwanao wanayedai kuwa alipotezwa na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa polisi mwaka Jana.

Familia ya Bakari Mbwana mwanyota Mwenye Umri wa miaka 26 kutoka eneo Bunge la Likoni Kaunti ya Mombasa inadai  kuwa mwanao aliyekuwa akijihusisha na biashara ya bucha alichukuliwa kutoka nyumbani kwake na watu waliyokuwa wamejihami mnamo usiku wa tarehe ishirini tatu mwezi Februari mwaka Jana na Hadi kufikia sasa bado hawajapata ripoti kuhusu aliko.

Kulingana na Mbwana Mwanyota ambaye ni Baba wa muathiriwa juhudi za kumtafuta mwanawe bado hazijazaa matunda licha ya  kumtafuta katika makafani mbalimbali sawia na kupiga ripoti katika baadhi ya vituo vya polisi nchini.

Aidha ameonyesha matumaini ya kumpata mwanawe akiwahai Kutokana na  agizo la rais William Ruto kuvunjwa Kwa   kitengo cha Huduma maalumu Katika idara ya DCI, akisema huenda hatua hiyo ikasaidia kuachiliwa Kwa mwanaye kutoka mikononi mwa maafisa wa kitengo hicho.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Baraza la maimamu na wahubiri hapa nchini CIPK sheikh Muhammad Dor ameipongeza hatua hiyo ya rais William Ruto kuondoa kitengo hicho, akimhimiza mkurugenzi mpya wa jinai Amin Mohamed kushirikiana na taasisi nyingine za kiusalama Nchini na kutoa taarifa kamili kuhusiana visa vyote nya wakenya waliopotezwa katika njia tatanishi.

https://eechicha.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287