Kalonzo kuhudhuria sherehe ya uapisho wa Abdulswamad

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Abdulswamad Shariff Nassir kuwa gavana mpya wa kaunti ya Mombasa hapo kesho
Kulingana vyanzo vya habari kutoka chama cha Wiper, Kalonzo anatarajiwa kuwasili Mombasa alasiri ya leo kwa ajili ya sherehe hiyo itakayoandaliwa hapo kesho katika bustani ya Mama Ngina Water Front.
Hatahivyo leo asubuhi gavana mteule wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir alizuru eneo hilo kutathmini maandalizi ya Kwa ajili ya siku hiyo ambapo aliwataka wakaazi wa Mombasa kujitokeza kwa wingi na jumuika kwenye sherehe hiyo.
Itakumbukwa kuwa mnamo siku ya jumatatu mwenyekiti wa kamati ya kusimamia sherehe hiyo Joab Tumbo alidokeza kuwa wanatarajia zaidi wakaazi 2000 kuhudhuria sherehe hizo.