Shallo aelekea mahakamani kupinga ushindi wa Machele

Aliyekuwa mgombeaji wa kiti cha Ubunge katika eneo la Mvita  kupitia chama cha UDA  Omar Shallo ameelekea mahakamani kupinga kuchaguliwa kwa  Mohamed Machele   kuwa Mbunge wa eneo hilo .

Kupitia kwa stakabadhi alizowasilishwa mahakamani, Shallo anadai kuwa uchaguzi wa Agosti tarehe tisa ambao ulimpa ushindi Machele aliyegombea na  chama cha ODM, uligubikwa na kasoro nyingi  ikiwemo visa vya kuhonga wakipiga kura ili kumchagua.

Aidha anadai kuwa licha ya baadhi ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa kuchelewa, tume ya kusimamia uchaguzi IEBC  haikufidia mda uliyopotea wakati wa  zoezi hilo, jambo ambalo anasema kuwa liliwakanganya wapiga kura wengi  waliyojitokeza  kushiriki zoezi hilo.

Wakati huo huo mlalamishi anadai kuwa uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki kwani vituo vingi vya kupigia kura  ambavyo vilikuwa katika ngome zake za kisiasa vilikumbwa na ghasia zilizoelekezwa kwa mawakala ,wasimamizi wa uchaguzi pamoja na maafisa wa usalama ili kutatiza zoezi hilo kwa makusudi.

Itakumbukwa kuwa machele alitangazwa mshindi na  IEBC katika kinyang’anyiro hicho  baada ya kuibuka na  kura 22,611 huku akifuatwa na  Shallo aliyepata kura 11,125.

https://boltepse.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287