Raia wa Jordan waliyokamatwa Mombasa wakiomba waregeshwa kwao
Raia arubaini wa Jordan waliokamatwa na maafisa wa polisi wiki moja iliyopita mjini Mombasa wakiomba katika mtaa wa Old Town wameregeshwa nchini mwao.
Watalii hao ambao walikamatwa kwa kosa la kukiuka sheria katika stakadhi zao za visa wanajumuisha watu wazima 19 pamoja na watoto 21, mdogo wao zaidi akiwa na umri wa miezi minne.
Hatahivyo akiongea na wanahabari mjini Mombasa wakati akisisimamia safari ya watalii hao Mwakilishi wadi wa eneo la Tudor Samir Balo amedokeza kuwa msaada wa usafiri waliyoupata raia hao wa Jordan Umetoka kwa mfanyibiasha tajika mjini Mombasa Hasu Patel ambaye aliingilia kati baada ya kusikia masaibu waliyokuwa wakipitia raia hao wa kigeni.
Awali maafisa kutoka idara ya uhamiaji na makachero kutoka kitengo cha kukabiliana na ulanguzi wa binadamu walikuwa wamewahoji raia hao wa kigeni lakini bado kufikia sasa hawajatoa ripoti kamili kuhusu uchunguzi wao.
Raia hao wanatarajiwa kusafari hadi Nairobi na kisha kuabiri ndege hadi nchini Jordan hapo kesho.